Hadi hivi sasa zaidi ya watu 14 elfu
wameshauawa na makumi ya maelfu ya wengine kujeruhiwa katika
mashambulizi ya kivamizi yaliyoanzishwa na Saudi Arabia na kundi lake
mwezi Machi 2015 dhidi ya taifa maskini la Yemen.
Aidha mamilioni ya
watu wamekuwa wakimbizi huku watoto wakiwa ndio wahanga wakuu wa jinai
hiyo. Abdallah Shaaban, mwanaharakati wa kupinga mzingiro dhidi ya Yemen
anasema kuhusiana na suala hilo kwamba:
Mtoto mmoja wa Kiyemen huaga dunia kila baada ya dakika kumi kutokana na maradhi mbalimbali.
Saudi Arabia ambayo ni dhihirisho la
Uwahabi na muenezaji wa itikadi potofu za kitakfiri na kisalafi kwa
kuwauwa watoto imeonyesha kuwa, haina mpaka wowote katika kutenda jinai
na kwa kushadidisha jinai zake hizo inataka kuthibitisha utambulisho
wake wa utumiaji mabavu. Utendaji huu ni kama utumiaji mabavu wa Kinazi,
Ufashisti na Uzayuni katika uga wa mahusiano ya kimataifa.
Licha ya
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF kukiri wazi juu ya matokeo
mabaya ya mashambulio ya anga ya muungano unaoongozwa na Saudia dhidi ya
raia wa Yemen hususan watoto,
Umoja wa Mataifa si tu kwamba,
haujachukua hatua yoyote ya maana ya kuhitimisha mashambulio hayo, bali
hadi sasa Baraza la Haki za Binadamu la umoja huo halijaunda tume huru
ya kimataifa kwa ajili ya kuchunguza jinai za Wasaudia.
Hivi karibuni Uholanzi ikiziwakilisha nchi kadhaa za Ulaya
ilipendekeza mpango wa kuundwa kamati ya kimataifa ya kuchunguza jinai
za Saudia huko Yemen ambapo utawala wa Riyadh ukipata uungaji mkono wa
Marekani na Uingereza uliuzuia mpango huo. Kabla ya hapo pia, Umoja wa
Mataifa ulitoa ripoti ambayo iliiweka Saudia katika orodha nyeusi ya
nchi zenye kukiuka haki za watoto kutokana na kushambulia kwa mabomu
shule na hospitali za Yemen.
Ripoti hiyo ilieleza kwamba, muungano wa
kijeshi unaoongozwa na Saudia huko Yemen unabeba dhima ya vifo vya
watoto na majeruhi wa nchi hiyo mwaka uliopita. Hata hivyo baada ya siku
chache tu tangu kutolewa ripoti hiyo, Ban Ki-moon aliyekuwa Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa wakati huo alilitoa jina la Saudia katika orodha
hiyo nyeusi ya nchi zinazokanyaga na kukiuka haki za watoto kwa hoja
kuwa, Riyadh ilitishia kwamba, kama jina lake halingeondolewa katika
orodha ya nchi hizo zinazokiuka haki za watoto, ingekatisha misaada take
ya kifedha kwa umoja huo.
Licha ya kuwa, katika kipindi cha
uongozi wa Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa yaani Antonio Guterres,
Saudia imewekwa tena katika orodha hiyo nyeusi kufuatia mashinikizo ya
fikra za waliowengi, lakini katika kipindi hiki pia hakujachukuliwa
hatua au kutekelezwa mashinikizo yoyote dhidi ya nchi hiyo. Mambo
yanaendelea kama vile hakuna jinai yoyote iliyofanywa na Saudia.
Muamala na utendaji huu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na jinai za
Saudi Arabia huko Yemen, unaonyesha kuwa, taasisi hiyo imegeuzwa na
kuwa klabu ya matajiri na watu wenye ushawishi ambapo jambo muhimu
kuliko yote ni kulindwa maslahi yao.
Kama ambavyo Umoja wa Mataifa
haukuchukua hatua yoyote dhidi ya utawala vamizi wa Israel ambao
ulifanya mashambulio mtawalia katika maeneo ya Wapalestina ukiwemo
Ukanda wa Gaza na kufanya mauaji ya maelfu ya raia wakiwemo watoto
wadogo.
Kwa hakika uungaji mkono huu ndio ambao
licha ya kutolewa indhari nyingi na baadhi ya asasi na makundi katika
Umoja wa Mataifa kuhusiana na hali mbaya ya kibinadamu, umepelekea
indhari hizo kutokuwa na dhamana ya kufanyiwa kazi.
Kiujumla Umoja wa
Mataifa si tu kwamba, haujatekeleza jukumu lake la kulinda amani na
usalama wa kimataifa, bali misimamo yake ya kindumakuwili na ya upande
mmoja imechangia kuendelea jinai za Saudia dhidi ya watu wa Yemen
hususan watoto wadogo.
chanzo:parstoday.
Comments