Kocha wa united jose mourinho amekiri kuwa wanaitaji kutumia pesa nyingi kwa ajili ya kukiunda upya kikosi chake.
Kitu kimoja ni klabu kubwa na jambo jingine ni timu kubwa ya soka. Ni mambo mawili tofauti, "Mourinho aliwaambia waandishi wa habari.
"Ni mwaka wa pili sasa tunajaribu kujenga upya timu ambayo siyo moja ya timu bora zaidi duniani. Manchester City walimnunua beki wa kulia kwa bei ya mshambuliaji. Unapozungumzia kuhusu klabu kubwa za soka, unazungumzia kuhusu historia ya klabu. "
Wakati ilipogusia kuwa United imetumia paundi milioni 286 chini ya Mourinho, Mreno huyo alisema: "Sawa, (lakini) haitoshi .. Bei ya klabu kubwa ni tofauti na klabu nyingine. kwa kawaida timu kubwa huadhibiwa katika soko kwa sababu ya historia yao. "
United sasa hawajafanikiwa kushinda katika mechi zao 3 za mwisho katika mashindano yote na wataikaribisha Southampton siku ya Jumamosi huko Old Trafford.
Comments