Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) tarehe 14 Disemba,2017 tumepokea
taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa Mbunge wa Siha Dr.Godwin
Mollel amejiuzulu uanachama na kujiunga na CCM .
Dr.Godwin Mollel ameeleza sababu ya uamuzi wake huo ni kutaka kulinda rasilimali za Taifa.
Sababu
hii aliyoitoa ni ya kushangaza kwani Bunge ndicho chombo chenye wajibu
wa kusimamia na kulinda rasilimali za Taifa kwa niaba ya wananchi.
Ni
jambo la kushangaza kwa kuwa kitendo chake cha kulikimbia Bunge kama
chombo cha kusemea na kutetea rasilimali za Taifa na kuja uraiani inatoa
taswira gani maana kalikimbia Bunge lenye wajibu huo kwa mujibu wa
Katiba na Sheria za nchi yetu.
Tunawashauri
wale wote ambao wanajitoa waeleze sababu halisi na sio kuhadaa umma kwa
sababu uchwara kama hizi, maana wapo wanaosema wanaacha kazi kwenda
kuunga mkono dhana ya ‘hapa kazi tu’ na wengine wanasema wanaenda kuunga
mkono juhudi za kuboresha maisha kwa kuacha kazi.
CHADEMA
tuko imara sana na tutaendelea na ajenda zetu bila kuyumbishwa na wimbi
hili la watu wachache ambao wameamua kuwasaliti wapiga kura wao kwa
kutoa sababu zisizo za msingi ambazo hazina maslahi kwa Taifa bali kwa
maslahi yao binafsi . Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.
Tutaendelea
kujenga Taifa letu na Chama chetu bila kujali njaa za baadhi yetu wala
maslahi ya watu wachache. Ila kwa hakika ni kuwa wale wenye dhamira
thabiti ndio wataweza kufika mwisho wa safari ya kuleta mabadiliko
salama. Ni dhahiri wale waliotanguliza ubinafsi hatutaweza kufika nao
mwisho wa safari hii.
Imetolewa Alhamis 14 Novemba, 2017 na ;
John Mrema,
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments