Jumuiya ya Maimamu Zanzibar JUMAZA imesikitishwa na amri ya kusitishwa kwa maandamano walikusudia kufanywa na Jumuiya hiyo pamoja na asasi mbalimbali za wanaharakati wa kupinga masuala ya udhalilishaji wa kijinsia.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika Ofisi ya jumuiya hiyo Vuga Mjini Zanzibar Katibu wa Jumaza Muhidin Zubeir Muhidin amesema kusitishwa kwa maandamano hayo kumewakosesha fursa ya kutoa Elimu ya kuachana na vitendo vya Udhalilishaji katika jamii.
Amesema pindipo maandamano hayo yangeruhusiwa kufanyika ingesaidia kwa kiasi kikubwa kuangalia namna ya kupinga na kujiepusha na vitendo vya audhalilishaji vinavyo leta madhara katika jamii hususani kwa wanawake na watoto.
Aidha ametowa wito kwa wananchi kuzidi kuripoti kesi za udhalilishaji zinazotokea katika jamii ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria pamoja na kuendelea kufuata sheria za nchi ili kuendeleza amani iliopo katika Nchi
Akisoma risala iliyokusudiwa kuwasilishwa katika Maandamano hayo Mjumbe katika kitengo cha kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia cha Jumuiya ya Maimamu Zanzibar JUMAZA Halima kassimu Muhammed ametowa wito kwa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kusimamia mavazi ya heshima kwa wananchi ili kupunguza vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia vinavyoendelea katika jamii.
Amesema pindipo wananchi wataekewa sheria na kusimamiwa katika mavazi ya heshima itasaidia kupungua kwa vitendo hivyo katika jamii.
Aidha amesema kwa kiasi kikubwa wananchi wa kike na wakiume wamekuwa wakivaa mavazi yasiyo na heshima wala yasiendana na maadili yao jambo ambalo linaleta ushawishi wa kuendelezwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia katika jamii.
Nae mwanaharakati wa katika taasisi za kidini Amina Yussuf Ramadhan amesema ni vyema kwa serikali kuendelea kuunga mkono juhudi za Jumuia za kiislam na Jumuiya za wanaharakati katika kuukemia masuala ya Udhalilishaji wa kijinsia ili kuondoa tatizo hilo Nchini.
Amesema wanawake ni miongoni na watu wanathiriwa na vitendo vya udhailisjai hivyo si vyema kwa serikali kushindwa kuwaunga mkono pindipo wanapotaka kuungana na wanawake wengine katika kupinga vitendo hivyo.
’’tunafanya yote haya kwa kufuta miongozo ya serikali kupitia Wizara ya kazi ,Uwezeshaji,Wazee,Vijana, Wanawake na Watoto lakini tunavunjika moyo kutokana na elimu tunayopewa tunashindwa kufikisha sehemu husika’’alisema Amina Yuusuf
Maandamano hayo yalikusudiwa kufanyia jana disemba2 2017,lakini yalihairishwa na kushindwa kufanyika jambo ambalo limerujesha nyuma shughuli za maendeleo ya JUMAZA pamoja wanaharakati wa maswala ya kijinsia.
chanzo:zanzibar24.
Comments