Jeshi la Polisi latoa tahadhari katika kipindi hichi cha skukuu kwa wananchi na madereva hasa hasa T-One.

Akizungumza na Waandishi
wa Habari Kamanda Hassan Nassiri amesema Jeshi lipo imara kuhakikisha
linadhibiti na kulinda amani za wananchi pamoja na mali zao katika
kipindi hichi cha sherehe za Krismasi na mwaka mpya.
Amesema mwananchi yeyote
atakaejihusisha na matendo ya uvunjifu wa amani endapo watatiwa nguvuni
na jeshi hilo hatua kali watachukuliwa dhidi yake.
Aidha Kamanda Nassir amewataka waendesha vyombo vya moto wanaojulikana kama T-One
kutoitumia fursa hiyo kwa kushangiria kwa fujo za kuendesha vyombo vyao
kwa mwendo wa kasi katika mizunguko ya mikutano ya barabara kama
Roundi ya bauti.
Hata hivyo amesema
ulinzi utaimarishwa katika makanisa yote yatakayofanyika ibada pamoja na
viwanja vyote vitakavyotumika katika kusherehekea skukuu hizo mbili.
Sambamba na hayo ametoa
wito kwa jamii kuwacha tabia ya kuchora barabara katika kipindi hichi
kwani hali ile inachafua miundombinu ya serikali.
chanzo: zanzibar24.
Comments