Bahram Qassemi amesema ni jambo la kutamausha kuiona Saudia inalipiza
kisasi kwa raia wasio na ulinzi, kutokana na kushindwa kwake katika
medani za vita.
Amesema mashambulizi haya ya kiwendawazimu yanayofanywa na Saudia kwa
kutumia silaha za Marekani ni ya kusikitisha na yanafanyika mbele ya
kimya cha jamii ya kimataifa.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Yemen, mashambulizi hayo ya anga
ndani ya masaa 48 yaliyopita katika wilaya ya Heime nchini Yemen
yamesababisha mauaji ya watu 71 huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa.
Msemaji wa harakati ya Ansarullah ya Yemen, Mohammad Abdulsalam
amelaani hujuma hizo dhidi mkusanyiko mkubwa wa raia wasio na hatia
sokoni na kusisitiza kuwa, hatua hiyo inaashiria kufeli kwa njama na
matarajio ya Saudia huko Yemen.
Katika hatua nyingine, ndege za kijeshi za Saudia zimetekeleza
mashambulizi ya anga dhidi ya makazi ya watu katika mkoa wa Hudaydah na
kuua watu 14 wa familia moja.
chanzo: parstoday.
Comments