Taarifa ya Gadi ya Pwani ya Italia imesema wahajiri hao waliokuwa
kwenye boti moja ya mpira na mbili ndogo za plastiki wameokolewa katika
operesheni zilizofanyika kati ya Jumatatu usiku na jana Jumanne.
Siku chache zilizopita, Kikosi cha Jeshi la Majini la Libya kiliokoa
wahajiri karibu 200 katika pwani ya magharibi mwa nchi hiyo katika
bahari ya Mediterania waliokuwa wakielekea Ulaya.
Libya imekuwa ikitumiwa kama nukta ya kuanzia safari za wakimbizi na wahajiri vijana wa Kiafrika kuelekea Ulaya.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2017 hadi sasa, karibu wakimbizi elfu
tatu wameaga dunia wakijaribu kufika Ulaya kupitia Bahari ya
Mediterania, vifo ambavyo vingi vimetokea katika njia ya bahari kutoka
Libya kuelekea Italia.
Mwaka uliopita, zaidi ya wahajiri elfu tano aghalabu yao wakiwa wa Kiafrika walipoteza maisha katika safari hizo hatari.
chanzo: parstoday.
Comments