
Vurugu kati ya wabunge na vikosi vya usalama zilitokea jana wakati muswada huo ulipoanza kujadiliwa.
Mwandishi wa BBC Catherine Byrahunga anasema sasa nchi inasubiri kuona namna ambavyo wabunge hao watapiga kura katika swala hilo nyeti la kubadilisha katiba.
Mipango ya kutoa ukomo wa umri wa Rais umepelekea kuwa na maandamano nchini Uganda.
Wengi wanaona kama mpenyo wa Yoweri Museveni kuwa Rais wa maisha.
Wakati huo huo , wafuasi wake wanasema kuwa wanaweza kupigia kura ya kumtoa wakati wowote. Lakini wapinzani wanahisi kuwa uchaguzi nchini Uganda haujawahi kuwa huru na hautakuwa huru kwa siku za usoni.

Chanzo:BBc.
Comments