Bailey amewahi kutajwa kuingia kwenye rada za Manchester United - ambao walitaka kumsajili mchezaji huyo wa miaka 20 kabla hajajiunga na Leverkusen Januari, wakati Chelsea ikiaminika kuwa ilikataliwa ofa ya paundi ya milioni 22 kwa ajili ya mshambuliaji huyo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa The Mirror, bosi wa Arsenal, Arsene Wenger anamkubali sana Bailey na atashinikiza kukamilisha dili la paundi milioni 30 kwa ajili ya Mjamaika huyo.
Bailey amefurahia miezi michache Leverkusen, akiwa amefunga magoli sita na sare nne za magoli katika mechi 14 Bundesliga.
Hata hivyo, Klabu hiyo ya Ujerumani bado inaendelea kuwa sehemu ya maendeleo kwa mustakabali wa mchezaji huyo kwani bado amebakiwa na miaka minne na nusu kwenye mkataba wake.
Comments