Ansarullah kuishambulia Somaliland ikiendelea kushirikiana na UAE dhidi yake.

Ansarullah kuishambulia Somaliland ikiendelea kushirikiana na UAE dhidi yakeHarakati ya Ansarullah ya Yemen imesema ikilazimu, itaishambulia jamhuri iliyojitangazia uhuru ya Somaliland kutokana na hatua yake ya kushirikiana na Umoja wa Falme za Kiarabu dhidi ya wapiganaji wa harakati hiyo ya Houthi.

 Harakati ya Ansarullah ya Yemen imesema ikilazimu, itaishambulia jamhuri iliyojitangazia uhuru ya Somaliland kutokana na hatua yake ya kushirikiana na Umoja wa Falme za Kiarabu dhidi ya wapiganaji wa harakati hiyo ya Houthi.

Taarifa ya Ansarullah imesema kuwa: "Iwapo Somaliland itatekeleza azma yake ya kuipa Imarati bandari ya Berbera iitumie katika mashambulizi yake dhidi yetu, tutajibu mapigo kwa kuvurumisha makombora ya balestiki dhidi ya eneo hilo lililojitangazia uhuru na mamlaka ya ndani nchini Somalia."

Mapema mwaka huu, serikali kuu ya Somalia mjini Mogadishu ililaani hatua ya bunge la Somaliland ya kuafiki mpango wa Imarati wa kutaka kujenga kambi ya kijeshi katika mji wa Berbera na kuitahadharisha Abu Dhabi kuwa Somalia itaifungulia mashtaka UAE kwa kukiuka sheria za kimataifa.

Mpango huo wa Imarati wa kutaka kujenga kambi yake ya kijeshi huko Somaliland umepingwa na nchi jirani zikiwemo Ethiopia na Djibouti.

Jamhuri ya Somaliland ilijitenga na Somalia mwaka 1991 na kisha kuutangaza mji wa Hargeisa kuwa mji  mkuu wake.chanzo:parstoday.

Comments