
Wakizungumza na Zanzibar24 Baadhi wa Wananchi wa kilimani,Amani
Fresha na Migomban wamesema kila mwaka hufika katika mahakama ya vileo
kupinga maombi ya wamiliki wa baa lakini mahakama hushindwa
kuyaskiliza maombi hayo na kuwapa kipaumbele wenye mabaa ya kuuza
pombe.
Hata hivyo wananchi hao wameiomba Mahakama ya vileo Zanzibar kuacha
tabia ya kuwabeba wamiliki wa baa, kwa kujali fedha wanazotoa kulipia
kibali cha pombe badala yake kuwatizama wananchi kwa jicho la huruma
kwani baa hizo zimekuwa zikileta athari katika jamii.
Wamesema mbali na kuuza pombe lakini pia hupiga miziki kwa sauti
kubwa bila ya kuzingatia mida ya sala,kuchafua mazingira katika maeneo
ya wananchi kwa kumwaga ovyo taka zao ikiwemo chupa na kondom
zilizotumika.
Hata hivyo wamesema kuwepo kwa hali hiyo imechangia kwa kiasi
kikubwa kuporomoka kwa maadili ya vijana na watoto katika jamii kwani
inapelekea kuiga matendo wanayoyaona kupitia baa hizo.
Aidha wametoa wito kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuziondoa baa
zote zilizojengwa karibu na makaazi ya wananchi ili kunusuru vizazi
visiweze kupotea pamoja na kunusuru afya za wananchi.
Jumla ya Baa tano leo Pia zilifika Mahakamani kwerekwe kwa ajili ya kufikisha maombi ya kibali cha pombe cha mwaka 2018.
chanzo:
Comments