Udom yapitisha sera kuwabana wezi wa kazi za kitaaluma.



Image result for udom
Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limepitisha sera ya haki miliki za kitaaluma.
Imeelezwa sera hiyo inalenga kuwabana wezi wa kazi za kitaaluma, kuboresha utafiti na uvumbuzi kwa kutoa uhakika wa haki za watafiti.
Akizungumza katika mahafali ya nane ya chuo hicho leo Jumatano Novemba 22,2017 mwenyekiti wa baraza hilo, Gaudentia Kabaka amesema sera hiyo itasaidia na kuboresha utafiti na uvumbuzi kwa kutoa haki za watafiti, wanafunzi na wahisani wengine katika shughuli zinazohusu chuo hicho.
“Sera hii inalenga kuweka bayana masuala ya ugawanaji wa haki miliki za kitaaluma na kutambua mchango wa watafiti, wanafunzi,
wahisani, wadau na chuo utokanao na mauzo ya haki miliki za kazi za uvumbuzi,” amesema.
Kabaka amesema baraza pia limepitisha mpango wa kukipandisha hadhi kituo cha afya cha chuo hicho kuwa hospitali. Alisema utaratibu umeanza kuhakikisha azma hiyo inafikiwa.
“Tunawakaribisha wananchi waweze kupatiwa huduma katika kituo chetu cha afya kilichopo hapa Udom,” amesema Kabaka.
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula amewaonya wahitimu kuacha
kuwa sehemu ya walalamikaji na badala yake kutumia fursa zilizopo kujipatia ajira.
chanzo:Mwananchi.

Comments