Shoti ya umeme yateketeza nyumba Zanzibar.

Nyumba inayomilikiwa na Bi Tupe Khamis imeungua kwa shoti ya umeme huko magogoni Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Wakaazi wa nyumba hiyo wameeleza kuwa  walipokua wamekaa ukumbini waliweza kusikia mlio mkubwa wa kitu kilichopasuka baada ya hapo ndipo walipoona moto uliokua umeanzia sehemu ya chumbani baada ya hapo ndipo uliposambaa nyumba nzima.

Wameeleza kuwa ndani ya vyumba hiyo vilivyowaka moto ni vyumba vitatu, magodoro matano,vitanda vitatu, makochi  viti vyakulia, nguo zote zilizokuepo ndani pamoja na kuathiri nyumba yote kwa ujumla.
Kwaupande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Hassan Nassir Ali ametoa wito kwajamii kuwa na utaratibu wa kuangalia mara kwamara miundombinu ya umeme katika nyumba zao ili inapotokea madhara ya yawe siyakuleta athari kubwa.
Akizungumza na na waandishi wa habari Mjumbe wa shehia ya Magogoni Salmini Subira amewapa pole waliokutwa na tatizo hilo na kuwataka wawe nasubira pamoja na uvumilivu.
chanzo:zanzibar24.

Comments