
Akiongea kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari Ndg. Polepole
amesema kuwa Chama chao kinalinda misingi na Itikadi zake ambazo ni
kuheshimu utu wa mtu pamoja na kuwatumikia raia hivyo kwa kiongozi
ambaye hawezi kufanya hayo lazima atakimbia.
“Mimi kama Katibu wa Itikadi na Uenezi sijawahi kutoa
tamko la kumsema vibaya mwanachama anayehama chama chetu kwasababu sio
misingi na Itikadi zetu”. Pia ameongeza kuwa ni dhambi kubwa kumhukumu mtu anapohama chama kimoja kwenda kingine.
“Hatuna tabia ya kuwasema vibaya wale wanaokihama chama,
lakini tumegundua kwamba raia wa kawaida ndio wamekuwa na tabia ya
kuwasema kwa sababu wanayaona matendo yao ya kutotosheka”, amesema Polepole.
Aidha Polepole amesisitiza kuwa CCM kwasasa imeweka misingi migumu
itakayowabana wasiotosheka na wasio na kiasi ndio maana tumeamua kuweka
sheria ya mtu mmoja, cheo kimoja. Sheria ambayo itawabana wenye kutaka
vyeo vingi kwa wakati mmoja.
chanzo:zanzibar24.
Comments