Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametoa miezi 12 kwa Kampuni ya Ranchi za Taifa (Narco) kukamilisha ujenzi wa machinjio ya kisasa ya Ruvu Bagamoyo mkoani Pwani.
Amemwagiza Kaimu Meneja Mkuu wa Narco, Profesa Philemon Wambura kutafuta fedha za kukamilisha ujenzi huo uliokwama kwa zaidi ya miaka mitano.
Wambura amesema ujenzi wa machinjio hayo ulianza mwaka 2009 na uliwekwa jiwe la msingi na Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete mwaka 2010 na ungegharimu Sh10.7 bilioni hadi kukamilika.
Hata hivyo, mwaka 2012 ujenzi ulisimama huku Sh2.7 bilioni zikiwa zimeshatumika.
Amesema kampuni ya Suma JKT ilipewa mkataba wa ujenzi ambao ulivunjwa mwaka 2012 kwa sababu kadhaa ikiwemo ramani ya mchoro wa jengo kutokidhi kiwango.
Baada ya taarifa kutolewa, waziri Mpina ameagiza kupatiwa maelezo ya kina ikiwa ni pamoja na nyaraka.
“Nawaagiza fanyeni liwezekanalo mpaka kufikia Desemba 2018 machinjio haya ujenzi uwe umekamilika na yaanze kufanya kazi," amesema.
Pia, ameagiza uongozi Narco kuongeza idadi ng'ombe kutoka 1,530 kufikia 4,000 kulingana na ukubwa wa eneo la ardhi lililopo la hekta 44,012.
Katibu Tawala Wilaya ya Bagamoyo, Erika Yegela amesema kutokana na ushirikiano uliopo kati ya halmashauri na uongozi wa
Narco watahakikisha maagizo yote wanayafanyia kazi kwa wakati.
chanzo:Mwananchi.
Comments