Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed
Dewji amepongeza uamuzi wa Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kufufua viwanda ambavyo
vilikuwa havifanyi kazi.
Dewji
ametoa pongezi hizo wakati akizungumza katika mkutano wa siku mbili wa
Global Business Forum 2017 (GBF) kuhusu Viwanda kwa Nchi za Afrika
uliofanyika Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).
Mfanyabiashara
huyo ambaye anamiliki viwanda 41 alisema uamuzi aliochukua Rais
Magufuli ni mzuri hasa katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaelekea
katika uchumi wa kati.
Dewji
alisema kampuni yake ya MeTL Group itaendelea kushirikiana na serikali
na katika kipindi cha miaka kadhaa ijayo amejipanga kuhakikisha anatoa
ajira kwa Watanzania 100,000 jambo ambalo litasaidia kukuza uchumi wa
nchi na kwa wananchi..
“Nianze
kwa kumpongeza Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa shabaha yake ya
viwanda, ni nzuri sababu kuna ongezeko la thamani lakini pia watu
wanaweza kupata ajira na pia hizi biashara zitalipa kodi ambazo
zitaisaidia serikali kuwekeza kwenye mambo ya afya na maji na huduma za
jamii. Mimi shabaha yangu kwenye miaka saba au nane ijayo MeTL Group
tunataka tuajiri watu 100,000,” alisema Dewji.
Dewji
ambaye kwa mujibu wa jarida la Forbes ni tajiri namba moja nchini
aliongeza kuwa utendaji wa Rais Magufuli ni wa kasi hivyo anategemea
kuwa katika kipindi cha miaka michache ijayo uchumi wa Tanzania utakuwa
umekuwa sana.
“Mimi
naona kwa kasi ya Mhe. Rais kwenye miaka miwili au mitatu ijayo
tutakuwa tumefika mbali sana, uchumi wetu kwasasa ni asilimia sita au
saba lakini kama tukitaka kuondoa umaskini lazima nchi yetu ukuaji wa
uchumi uanze kukua kwa zaidi ya asimilia 10, mimi nina muamini sana Mhe.
Rais na shabaha yake kwahiyo Mungu atutangulie na sisi tupo nyuma yake
tutafika hivi karibuni,” alisema Dewji.
Pia
Dewji alizungumzia umuhimu wa mkutano wa GBF ambao umekutanisha watu
kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wakiwepo viongozi wa serikali za
nchi za Afrika na wawekezaji alisema ni nafasi ya kipekee kwani pamoja
na kujadili viwanda pia amepata nafasi ya kuwaelezea washiriki wa
mkutano fursa za uwekezaji zilizopo hapa nchini.
“Umuhimu
ni mkubwa sana nakuja hapa kama MO lakini pia nawakilisha nchi yangu
Tanzania, nimeitangaza nchi yangu ili watu waje na wawekeze, nimewaeleza
mazingira yetu ya uwekezaji ni mazuri, tuna malighafi na tunahitaji
viwanda angalau watu wetu wa Tanzania wapate ajira na serikali ipate
kodi,” aliongeza Dewji.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments