Mhe. Makonda atembelea Ofisi za Clouds Media Group.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Paul Makonda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Dar es salaam ametembelea na kutoa pole katika Ofisi za Clouds Media Group baada ya Ofisi hizo kukumbwa na janga la moto hapo jana majira ya saa nne asubuhi.

Viongozi wengine wa serikali waliofika Ofisini hapo ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta.


Hata hivyo, Tayari matangazo ya vituo vya Clouds FM na Clouds TV vimerejea hewani baada ya kupotea siku nzima ya jana kutokana na hitilafu iliyosababishwa na moto huo ambao chanzo chake hadi sasa hakijajulikana.

chanzo: zanzibar24.

Comments