
Amesema serikali mkoani humo imelazimika kuchukua hatua kutokana na malalamiko mengi yanayotolewa na wananchi wa kijiji hicho dhidi ya muekezaji huyo juu ya vitendo vya unyanyasaji anavyowafanyia wanakijiji
vikiwemo vya kuwatishia kuwapiga pale ambapo wanapita karibu na maeneo ya fukwe ya Hoteli hio pamoja na kuwanyima haki zao wafanyakazi na kuwafukuza kiholela.
Mh. kitwana ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza katika kikao cha pamoja kilichowashirikisha maofisa kutoka kamisheni ya utalii na idara ya uhamiaji, uongozi wa wizara ya habari, kamati ya ulinzi na usalama na watendaji wa mkoa pamoja na wenyeji wa kijiji hicho chenye lengo la kulipatia ufumbuzi mgogoro huo.
Mhe. kitwana amesema lengo la Serikali la kukaribisha wawekezaji katika Sekta ya utalii ni kuleta maendeleo na sio kuleta migogoro na wanajamii hivyo amewataka wawekezaji kufuata sheria na taratibu za nchi pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayowazunguka ili kuona kwamba lengo la serikali linafikiwa.
Nae waziri wa habari utamaduni utalii na michezo mhe Rashid Ali Juma amewapongeza wananchi wa kijiji hicho kwa kuheshimu sheria na taratibu za nchi kwa kuzifikisha kero zao kwenye sehemu husika bila ya kufanya maamuzi ya kuchukua hatua yoyote mikononi mwao.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kati ndugu Mashavu Sukwa Said amewataka wananchi wa ukanda wa pwani kuwa makini wakati wanapouza maeneo yao kwa wawekezaji ili kuepusha athari mbali mbali zinazojitokeza ikiwemo kuathirika maeneo wanayotumia kwa kuzikana.
chanzo:zanzibar24.
Comments