
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo masauni amesema lengo ni
kupunguza changamoto ya makaazi kwa askari polisi kisiwani pemba, ambao
wamekuwa na hali ngumu katika makaazi yao licha ya kazi ngumu
wanazozifanya za ulinzi wa raia na mali zao.
Amesema serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania imetoa kipaumbele
kutatua changamoto za makaazi kwa askari polisi wa kisiwani pemba
dodoma na mikoa mipya kwa kutumia wadau ambao wapo tayari kungamkono
jitihada hizo.
Kwa upande wao wakuu wa mikoa ya kusini na kaskazini pemba mwanajuma
majid abdulla na omar khamis othman wamemshukuru naibu waziri huyo wa
mambo ya ndani kwa kuchukua juhudi za kutatua changamoto ya makaazi
inayokabili askari katika mikoa yao.
Zaidi ya familia 50 za askari polisi kisiwani pemba zitanufaika na
nyumba hizo zitakapomalizika, kati ya familia 400 wanaohitaji makaazi
ambapo mia 200 ni kutoka kusini na mia 200 kaskazini.
chanzo:zanzibar24.
Comments