Waziri
mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hana mpango wa kurejea CCM kama
ambavyo taarifa zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Lowassa
alisema jana Jumanne kuwa amepata taarifa za uvumi unaosambazwa kuwa
kuna watu amewatuma kuomba arudi CCM jambo ambalo ni uongo.
"Huu ni uongo wa kutunga, wamekuwa wakitunga vitu vingi juu yangu, mimi sina mpango wa kurejea CCM," alisema Lowassa,ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema .
Alisema
uongo mwingine ambao unasambazwa ni kuwa Serikali imezuia watu
kumtembelea nyumbani kwake jambo ambalo anaamini ni maneno yanayotungwa.
"Watu
wanazuiwa kuja nyumbani kwangu, eti Serikali imezuia hivyo wanakuwa
wanaogopa huu ni uongo Serikali haiwezi kuzuia watu kutembeleana," alisema.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments