Usalama umeimarishwa katika mji mkuu
wa Kenya Nairobi wakati wa siku ambayo rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa
kuapishwa kwa awamu ya pili ya urais.
Takriban viongozi 13 wa mataifa tofauti wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.
Kiongozi
wa upinzani Raila Odinga ambaye alisusia marudio ya uchaguzi ameitisha
kufanyika kwa mkutano wa upinzani licha ya mkutano huyo kupigwa
marufuku.
Uchaguzi wa mwezi Agosti ulifutiliwa mbali na mahakama kutokana na kile kilitajwa kuwa uchaguzi usio huru na haki.
Marudio
ya uchaguzi wa Oktoba 26 ulimpatia Uhuru Kenyatta asilimia 98 ya kura
huku waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo wakiwa asilimia 39.
Sherehe hiyo ya siku ya Jumanne inayofanyika katika uwanja wa
michezo wa Kasarani jijini Nairobi inatarajiwa kuanza mwenzo wa saa nne.
Waandalizi
wanatarajia watu 60,000 kujaza uwanja huo huku skrini kubwa zikiwa
zimewekwa nje ya uwanja huo kwa wale watakaoshindwa kuingia.
Naibu wa rais William Ruto, pia ataapishwa.
Miongoni mwa
viongozi wa kigeni wanaotarajiwa ni waziri mkuu wa Israeli Benjamin
Netanyahu, rais wa Uganda, Yoweri Museveni na rais wa Rwanda Paul
Kagame.
Upinzani nchini humo umewataka wafuasi wake kususia
sherehe hiyo na badala yake kukusanyika katika mkutano ili kuwakumbuka
wafuasi waliouawa katika ghasia tangu uchaguzi wa mwezi Agosti.
Maafisa wapolisi wameonya upinzani huo dhidi ya kufanya mkutano huo.
chanzo;Bbc.
Comments