Hiki ndicho alichosema RC Makalla Mbeya.

Kutokana na malalamiko ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla kuhusu habari iliyochapishwa na gazeti hili jana, ikimkariri kuwa ataandika barua kwa mwenyekiti wa CCM na katibu mkuu kutokana na chama hicho kushindwa katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Ibighi.
Mwananchi imechapisha maneno yaliyosemwa na Makalla kama ifuatavyo;
“Tutatiana moyo, tutapongezana lakini uchaguzi wa Ibighi doa kubwa kwa Mkoa wa Mbeya,” alisema.

“Nimejiuliza sana, tumekosea wapi? Tumekosea wapi mpaka watu wafike hawa wananchi, hili jambo msilibebe tu kirahisi rahisi, tusiibebe tu.
“Mimi nilitaka hiyo kata moja ingekuwa mkoa mwingine sio wa Mbeya. Tunapeleka meseji gani kwa uongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi.
“Kwamba kata moja, imeikataa CCM sio jambo dogo hili. Kwa hiyo viongozi mtakaochaguliwa leo wa UWT, hiyo iwe home work, namna gani tutarekebisha matatizo tuliyo nayo.
“Jiulizeni, wananchi wanafikaje kumchagua mtu ambaye mbunge wa jimbo ni wa CCM, Baraza la Madiwani walio wengi ni wa CCM, uamuzi utakaofanywa ni wa madiwani walio wengi wa CCM, wilaya ambayo kwa ngazi ya kitaifa yupo Naibu Spika ambaye anao uwezo wa kuwasemea watu wa Mbeya, watu wa Rungwe.
“Wilaya ambayo mkurugenzi anateuliwa na Serikali ya CCM, wilaya ambayo ina mkuu wa wilaya anayeteuliwa na Serikali ya CCM, mkoa ambao mkuu wa mkoa anateuliwa anatokana na Serikali ya CCM.
“Watu wanafika wanachagua tofauti wabaki kuwa wakiwa jiulizeni kuna tatizo gani?
“Mimi nimejiuliza sana, imeniuma sana kuna kazi ya kufanya. Hata hiyo kata lazima tungeichukua, sasa mimi niseme tunawaomba radhi wenzetu na makao makuu ya Chama cha Mapinduzi na mwenyekiti wetu. Lazima tufanye kazi ya tathmini ya kutosha ilipaswa this time iwe 43 ya 43 zote za Chama cha Mapinduzi.”
chanzo:Mwananchi.

Comments