
Mwalimu huyo aliyeuawa ametambulika kwa jina la Sergey Danilov inaelezwa kuwa alibaki darasani na kijana huyo wakati wanafunzi wengine wakiwa nje kwa mapumziko mafupi ya kifungua kinywa.
Baada ya kutekeleza mauaji hayo, Emelyanenkov alichukua simu yake na kupiga selfie na mwili wa marehemu uliokuwa umedondoka sakafuni kisha kusambaza picha hizo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Hata hivyo, baada ya muda mfupi alichukua msumeno wa moto (Chainsaw) na kujiua kwa kujikata koromeo.
Wanafunzi wenzake wameeleza kuwa Emelyanenkov alibakia darasani kwa mahojiano na mwalimu huyo baada ya kufanya vibaya kwenye somo lake na makosa mengine ya kinidhamu.
Tayari polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limetokea jana (Jumatano) asubuhi baada ya kutokea kwa vurugu kati yao na kudai kuwa bado upelelezi wa kina unaendelea.
Polisi wamesema walikuta video kwenye simu yake ikiwaonesha wawili hao wakigombezana na baadhi ya picha za Mwalimu huyo akiwa amelala sakafuni zikiwa zimepigwa na kutumwa kwenye makundi ya WhatsApp.
chanzo:zanzibar24.
Comments