Alichosema Mamaake Kanumba baada ya hukumu ya Lulu.

Mara baada ya mahakama kuu tanzania kutoa hukumu ya kifungo cha miaka miwili kwa muigizaji maarufu Lulu Michael ambaye ametenda kosa la kumuua steven kanumba bila ya kukusudia, Mama wa marehemu Steven Kanumba ameishukuru  mahakama na serikali kiujumla juu ya maamuzi waliyoyatoa kuhusu kesi hiyo.

“Mimi sina la kusem kwa sasa hivi ila la kwanza namshukuru mwenyezi mungu sana,pili ninaishukuru mahakama kwa kutenda haki na pia naishukuru sana seriakli yangu na hata nikitoka hapa nitaenda makaburini naamini  sasa naenda kumzika  na akapumzike kwa amani.” 


Aliongea Mama Kanumba huku akilia kwa sauti.

Lulu alikutwa na kesi hiyo mwaka 2012, ambapo alimuua Kanumba aliyekuwa mpenzi wake bila kukusudia kutokana na ugomvi wa mapenzi waliokuwa nao wawili hao ambapo katika purukushani hizo Kanumba alidondoaka na kuanguka chini na ndipo mauti yalipomkuta.
chanzo: zanzibar24.

Comments