
“Huu ni unyama umevuka kiwango kijana anathubutu kumbaka mtoto mdogo kama yule, sijui tunaelekea wapi vijana wa namna hii hawastahili kuishi na jamii,” alisema mmoja miongoni mwa wananchi Hussen Juma.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba,amesema tukio hilo limetendwa na kijana mmoja mkaazi wa kijiji cha Magamba juzi huko katika Kitongoji cha Komkola Chang’ombe.
Kamanda Wakulyamba alisema mtoto aliyebakwa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni akiendelea na matibabu na kwamba, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Alitoa wito kwa wazazi kutowaacha watoto wao kuzurura mitaani, ili kuwalinda wasitendewe vitendo vya kikatili kama hivyo.
chanzo:zanzibar24.
Comments