
Hii inafuatia ukosoaji mkubwa kutoka
kwa viongozi mbalimbali ulimwenguni, kutokana na uamuzi huo wa kumteuwa
Mugabe ambaye anayelaaniwa na watu wengi duniani.
Sasa Ghebreyesus, amesema kuwa atatoa taarifa mpya hivi karibuni kuhusiana na uamuzi huo.
Serikali
ya Uingereza inasema, imeshtushwa na kuvunjika moyo, kuwa shirika la
Afya Duniani, WHO, limemtaja rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, kuwa
balozi wa nia njema.
Msemaji mjini London, alieleza kuwa bwana Mugabe anakabili
vikwazo vya Marekani na Umoja wa Ulaya, na kuteuliwa kwake, kutaathiri
kazi za WHO.
Akifafanua uamuzi wa uteuzi huo , Mkurugenzi mkuu
mpya wa W.H.O, Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus, alisifu namna Zimbabwe
inavyozingatia afya ya umma.
Lakini wakosoaji wanasema katika
kipindi cha miaka thelathini na saba ya utawala wa rais Mugabe, huduma
za afya zimekuwa mbaya ambapo wahudumu wa afya wamekuwa hawalipwi mara
kwa mara , na kumekuwa na ukosefu mkubwa wa dawa muhimu .
Dr
.Tedros, ni raia wa Ethiopia ambaye ni Muafrika wa kwanza kuongoza
shirika la W.H.O. na alichaguliwa kwa ajili ya kukabiliana na kile
kilichoaminiwa kuwa ni kugeuzwa kwa shirika hilo kuwa la kisiasa.
chanzo:Bbc.
Comments