WAVUVI kisiwani Pemba, washauriwa kuitumia na kuifanyia kazi sheria ya Uvuvi namba.7, ya mwaka 2010.
Kaimu Afisa Mkuu idara ya
maendeleo ya Uvuvi Pemba, Ali Said Hamad, ameyasema hayo katika kambi maalum ya
kuwajengea uelewa wavuvi wadogo wadogo huko wesha Wilaya ya Chake Chake.
Afisa huyo amesema
kuwa, wavivi wote wanajukumu la kuisoma na kuifuta sheria na sera iliopo kwani
ukiukwaji wa sheria hio ndiko kunakochangia uharibifu wa mazingira ya bahari na
kupelekea uvuvi haramu.
Kwa upande wake, Afisa
Uvivi , Hidaya Khamis Hamad, amesema kuwa, sheria haikuekwa kuwakomoa wavuvi
bali ipo kutoa maelekezo sahihi yatakayoweza kumpatia mwanajamii mazao yenye
kiwango kinachostahiki kiuchumi na kipato zaidi.
Sambamba na hayo Afisa
Ufugaji , Ali Hatib, amewasisitiza wavuvi hao kuacha kutumia dhana za uvuvi
haramu na kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu kwa faida yao na vizazi
vijavyo.
Kwa upande wake,
Ramadhan Haji Ramadhan, amechangia kwa kusema kuwa, Serikali inapaswa kuangali
utaratibu wa kuwatafutia vyombo wavuvi wa Zanzibar ambapo zitasaidia kwenda
kuvua maji marefu jambo ambalo lisasaidia kutoa ajira kwa
wananchi waliowengi
hasa wanaoekeza katika rasilimali za bahari.
Aidha ameishauri
Serikali kupitia taasisi husika kuwaangalia zaidi walioekeza katika shughuli za
uvuvi wakati unaporuhusu kuona kuwa wanafaidika katika shughuli zao.
Comments