Watu wawili wafariki Dunia kufuatia ajali ya barabarani Unguja.

Watu wawili wafariki Dunia baada kupata ajali na mmoja amelazwa Hospitali ya Mnazi mmoja  kwa matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata kufuatia matukio tofauti ya ajali za barabarani.

Kwamujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini  Magharibi Kamishna msaidizi Muandamizi wa Polisi Hassan Nassir Ali amesema tukio la kwanza limetokea majira ya saa 3  Usiku
wa kuamkia jana huko amani kwa mabata baada ya gari isiyofahamika wala dereva kumgonga mwenda kwa miguu alie tambuliwa kwa jina la Kardudi Mambo mwenye umri wa miaka 35 mkaazi wa kwamabata na baadae na  gari hiyo kukimbia ambapo mpatwa na ajali alipata maumivu makali mwilini na kulazwa Hospitali ya Mnazi Mmoja na kufariki majira ya saa 2 asubuhi.

Tukio la pili limetokea jana majira ya saa10 Alfajiri huko Amani viwanda vidogo vidogo baada ya gari yenye namba za usajili  Z872GH aina ya Noha iliyokuwa ikitokea viwanja vya starehe umaarufu mjini joto kuacha njia na kupinduka.

Katika ajali hiyo Ameri Haji Makame mwenye umri wa miaka 20 mkaazi wa melinne Fuoni amefariki duninia na Maryam Madaraka Iddi mwenye umri wa miaka 25 mkaazi wa melinne amepata jeraha la kichwa na amelazwa Hospitali ya Mnazi mmoja kwa matibabu.

Hadi sasa Dereva pamoja na wengine waliokuwemo katika gari hiyo hawafahamiki walipo.
chanzo: zanzibar24.

Comments