Wanne kizimbani kwa kutaka kumuuwa Diwani.

WATU nane wakazi wa Ntyuka Manispaa ya Dodoma, wamefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Chamwino kwa tuhuma za kutuo maneno ya kutishia kumuua Diwani wa Kata ya Ntyuka, Theobale Emmanuel.
Kesi hiyo namba 234 ya mwaka 2017 inasikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo ya Chamwino, Zawadi Ndudumizi.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Ntyuka kinyume cha kifungu cha 89 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ambacho kilifanyiwa marejeo mwaka 2002.
Watuhumiwa hao ni pamoja ni Edward Lamoli, Edward Lauli, Petro Mjelwa, Yona Andrea, Lucas Mombo, Stephen Karashani, Zabron Leganga na Mussa Majana.
Hata hivyo, Washtakiwa wako nje kwa dhamana na kesi hiyo itasikilizwa tena Oktoba 24 mwaka huu.
chanzo:zanzibar24.

Comments