Wanafunzi wanne watiwa mbaroni kwa kutaka kuuwa mwenzao Geita.


Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Geita ACP Stanley Turiamo, amesema Wanafunzi wanne wa shule ya sekondari Geita wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kumpiga mwenzao na kumtishia kumuua.

Tukio hilo limetokea baada ya wanafunzi hao kumpiga mwanafunzi mwenzao wa kidato cha tano na kisha kumtishia kumuua hali iliyosababisha kuibuka kwa vurugu shuleni hapo.


ACP Turiamo ameendelea kusimulia kwamba licha ya vurugu hizo, wanafunzi pia waliwapiga kwa mawe bodi ya shule ambayo ilifika shuleni hapo kujadili suala lao, na kugomea kula kwa siku nzima.

chanzo: zanzibar24.

Comments