
Mwakilishi wa Nafasi za wanawake Mwantatu Mbarak Khamis amesema
kutokana na ufaulu mdogo kwa wanafunzi wenye ulemavu Zanzibar
kunakosababishwa na sababu mbalimbali ipo jana kwa serikali kutafuta
mbinu ya kuwasaidia vijana hao ili kupata elimu itakayowasaidia katika
kujenga maisha yao.
Akijibu swali katika kikao cha baraza la wawakilishi Naibu Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mmanga Mjengo Mjawiri amesema
Serikali imekuwa ikifanya kila njia ili kuwajengea wanafunzi wenye
ulemavu mazingira bora ya kujifunza ili kuweza kufanya vizuri katika
masomo.
Amesema serikali imekuwa ikiwasomesha walimu kwa ngazi mbalimbali
ikiwemo cheti,diploma na kuwajengea uwezo ili waweze kuwasaidia watoto
wenye mahitaji maalum kuweza kujifunza kupitia elimu mjumuisho
pamoja na kuwapatia vifaa vyote muhimu vya kufundishia.
Aidha Mjengo amesema Wizara yake itaendelea na jitihada za
kuimarisha elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum kwa kuajiri walimu
waliohitimu kozi ya shahada na stashahada ya elimu mjumuisho,Kuweka
miundombinu rafiki kwa watoto hao ikiwemo ujenzi wa ramps katika skuli
50 unguja na pemba.
chanzo: zanzibar24.
Comments