Shehia 6 zinazo ongoza kwa maradhi ya kichocho zanzibar.

kichochoMkuu wa kitengo cha maradhi yasiyopewa kipaombele Fatma Kabole amesema maradhi ya kichocho yamepungua kutoka asilimia 60 mnamo mwaka 80 hadi kufikia asilimia 1.7 kwa mwaka 2017.

Akizungumza na Waandishi wa habari baaada ya mkutano wa kuwasilisha ripoti ya utafiti wa Maradhi ya kichocho hapa Zanzibar amesema kupungua kwa maradhi kunatokana na mwamko wa wananchi kutumia dawa za kujikinga na maradhi hayo.


Wataalamu wamaliza maradhi ya kichocho Pemba

Amesema katika kuhakikisha maradhi hayo yanaondoka nchini Wizara ya afya itaendelea na juhudi za kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujinga na maradhi ya kichocho ikiwemo kuacha kutumia maji yaliotuama katika madibwi ambayo sio salama kwa matumizi ya binaadamu.

Amesema mbali na mafanikio hayo lakini kuna baadhi ya Shehia bado zinakabiliwa na maradhi hayo ikiwemo Chaani , Kitope na mwera kwa unguja na Chambani ,Uwandani na kitongoji kwa Pemba.

Aidha amesema katika kubabiliana na maradhi hayo wizara ya afya inaendeelea na juhudi za kutoa elimu ya kujinga na maradhi ya akichocho ikiwemo wananchi kutumia Vyoo ,kuacha kutumia maji ya mito badala yake watumie Maji safi na Salama ili kuepukana na maradhi hayo .

Utafiti huo umefanywa na Mradi wa SCORE ambao umeazishwa mwaka 2002 hapa Zanzibar ukiwa na lengo la kuangalia namna ya kupambana na maradhi ya kiichocho Nchini.

chanzo: zanzibar24.

Comments