
Rais Magufuli ameyasema hayo leo kwenye sherehe za uzinduzi wa daraja la Furahisha la mkoani Mwanza. “Tuliwatazama
watu wakajenga wakaweka ‘Investment’ zao, sasa leo tunawafukuza,
tusubiri kwanza, inawezekana walifanya makosa lakini kwa sababu serikali
yangu ina huruma nasema ndugu zangu msiwabomoleshe, yapo maeneo ambayo
kwa kweli itabidi watu wahame, mfano wale wa uwanja wa ndege, kama kuna
mahali pa kubadilisha sheria mimi nitazibadilisha ili kusudi baadhi ya
wananchi waliojenga pale miaka 30 tuweze kuwalinda na kukaa pale na
kuendesha maisha yao”, amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli leo yupo mkoani Mwanza kwenye ziara ya kikazi ya siku
mbili, ambapo pia licha ya uzinduzi wa daraja la Furahisha, anatarajiwa
pia kuzindua kiwanda kimoja.
chano: zanzibar24.
Comments