
Vicent Lissu, amesema mbunge huyo atahamishwa kutoka katika hospitali
hiyo kwenda kupata matibabu ya kibingwa zaidi kama ilivyoelezwa Jumanne
iliyopita na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Freeman Mbowe.
“Mheshimiwa Lissu bado anaendelea na matibabu kwenye
hospitali ileile,” Vicent alisema, “akihamishwa mtajua maana tutaeleza
ila kwa sasa bado ni mapema kusema atakwenda nchi gani, itoshe kujua
bado yupo Nairobi.”
Hadi jana jioni, dola za Marekani 31,663 (Sh. milioni 69.9) zilikuwa
zimechangwa na watu walio ughaibuni kugharamia matibabu ya Lissu, ikiwa
ni ongezeko la dola 1,969 (Sh. milioni 4.36) kutoka zilizokuwa
zimechangwa wakati Mbowe akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya
mwisho jijini Dar es Salaam kuhusu hali ya Lissu.
Kwa mujibu wa mtandao wa www.gofundme.com/Lissumedicalcare, tangu
utaratibu huo wa watu walio ughaibuni kumchangia Lissu uanzishwe
Septemba 12 na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, mtu
aliyetoa mchango mkubwa zaidi ni Yasinta Massawe aliyechangia dola 3,000
(Sh. milioni 6.6).
Mbowe aliwaambia waandishi wa habari Jumanne kuwa michango hiyo
imetokana na uhamasishaji unaofanywa na Watanzania walio nje wakiongozwa
na Mange Kimambi anayeishi Marekani.
Katika mkutano wake wa Jumanne, Mbowe alisema Lissu ambaye amefanyiwa
operesheni 17 hadi Oktoba 12, gharama za matibabu yake zilikuwa
zimefikia Sh. milioni 412.45.
“Hata mpaka sasa hivi bado fedha hazijatosha.
“Hapa ninazungumza gharama ya matibabu pekee yake kwa
mwezi Septemba zimegharimu fedha za Kenya Sh. 10,687,316 sawa na dola za
Marekani 106,875 na ilipofika Oktoba 12 jumla ya gharama ni Sh.
13,708,156 za Kenya.”
Mbowe pia alisema jopo la madaktari 12 ambao walikuwa wanamtibu Lissu
wamelipwa Dola za Marekani 46,440 (Sh. milioni 102.5) kwa kuwa kila
daktari anapotoa huduma kwa muda fulani anahitajika kulipwa.
chanzo: zanzibar24.
Comments