Mahakama yawapa onyo wanaofanya biashara ya vileo Zanzibar.

Mahakama ya Vileo zanzibar imesema itawachukulia hatua Kali za kisheria kwa kuwafungia biashara zao baadhi ya wafanyabiashara wa Vileo wanaofanya biashara kinyume na sheria bila ya kuwa na kibali wala lesseni zilizotolewa na Mamlaka husika.
Akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa baa katika mkoa wa kaskazini unguja Katibu wa Mahakama ya Vileo zanzibar Saleh Ali Abdalla
amesema endapo hawatawachukulia hatua mapema wataweza kuikosesha serikali mapato ambayo yanasaidia katika kuimarisha huduma za kijamii ikiwemo ujenzi wa barabara za ndani, Skuli,Hospital na Uchimbaji wa visima katika makaadhi ya wananchi.
Hata hivyo amesema katika ziara hiyo Mahakama imegundua kuna baadhi ya baa bado hazina viwango vya kuendelea kufanya biashara hizo kutokana mazingira yao hayaridhishi kwa kufanyia biashara hiyo.
Zaidi ya baa na hoteli 80 katika mkoa wa kaskazini zimefanyiwa ukaguzi na Mahakama ya Vileo zanzibar.
chanzo:zanzibar24.

Comments