Choe Son Hui amesema kuwa Marekani inafaa kujiandaa kuishi na Korea Kaskazini yenye silaha za kinyuklia.
Amesema kuwa ndio njia pekee ya kuwa na amani ya kudumu kati rasi ya Korea.
Mkurugenzi
wa shirika la kijasusi nchini Marekani Mike Pompeo awali alikuwa
ameonya kwamba Korea Kaskazini inaweza kuishambulia Marekani na kombora
la kinyuklia katika kipindi cha miezi michache ijayo.
Korea Kaskazini imesema kuwa tayari ina uwezo huo.
Bwana Pompeo amesisitiza kuwa Washington bado inataka kutatua
swala hilo kidiplomasia na vikwazo lakini ikasema inaweza kulazimika
kutumia nguvu.
Akizungumza katika kongamano la kuzuia kuenea kwa
silaha za kinyuklia mjini Moscow, bi Choe alisisitiza matamshi
yaliotolewa awali na maafisa wa Korea Kaskazini kwamba silaha za
kinyuklia ni swala la ''maisha na kifo'' kwa taifa hilo.
Mapema mwaka huu, aliripotiwa akisema kuwa taifa hilo liko tayari kufanya majadiliano na Marekani iwapo mazingira yataruhusu.
Lakini siku ya Ijumaa bi Choe alisema kuwa Korea
Kaskazini itaangazia utekelezwaji wa maamuzi ya vikwazo vya Umoja wa
mataifa akivitaja kuwa ni hatua ya uchokozi na vita.
Tangu Korea Kaskazini ilipoanza kufanyia majaribio makombora yake mwaka huu, vikwazo dhidi ya taifa hilo vimeongezeka.
Serikali
ya Australia ilisema siku ya Ijumaa kwamba ilipokea barua kutoka Korea
Kaskazini ambayo pia ilikuwa imetumwa kwa mataifa mengine ikiitaka
Australia kutoshirikiana na Marekani.
Siku ya Alhamisi bwana
Pompeo alionya kuwa makombora ya Pyongyang yalikuwa yanapiga hatua kwa
kasi hivyobasi kuwa vigumu kwa majasusi wa Marekani kuwa na hakika
kuhusu ufanisi wake, lakini akasema watagundua hivi karibuni.
chanzo:Bbc.
Comments