Taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya ACT-Wazalendo, Mohamed Babu imesema Zitto
amesafirishwa kwa gari saa 10:00 usiku akitokea kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA).
Amesema
kamati hiyo inafuatilia kwa umakini hatua kwa hatua kuhakikisha usalama
wake ikiwataka wanachama na wananchi kuendelea kuwa watulivu.
Katibu
wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema
Zitto amesafirishwa kwa gari la Bunge akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Zitto anatakiwa kufikishwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
chanzo:Mwananchi.
chanzo:Mwananchi.
Comments