Watendaji wa Hospitali ya Chake chake watoa ahadi mbele ya Afisa mdhamini Wizara ya Afya Pemba.

chakeAfisa mdhamini Wizara ya Afya Pemba Bakar Ali Bakar amewataka viongozi na watendaji wa Hospitali ya Chake chake kuwa na mashirikiano katika utendaji wao ili  kuipa  matumaini jamii juu ya  huduma zitolewazo na hosiptali hiyo.

Amesema katika siku za hivi karibuni kumekuwa na lawama ya ukosefu ya uwajibikaji kutoka kwa baadhi ya watendaji jambo linalorejesha nyuma juhudi za serikali za kuwaletea wananchi huduma za afya bora .


Bakari ameyasema hayo huko hospitali ya Chake chake wakati akizungumza na kamati ya uongozi ,madaktari na baadhi ya watendaji kufuatia malalamiko yanayotolewa na baadhi ya wagojwa wanaolazwa hospitalini hapo

Nao baadhi ya watendaji waliokuwa katika kikao hicho wamekiri kuwepo kwa mapungufu ya kibinadamu huku wakisema uchache wa wahudumu pia  huchangia kukosekana kwa huduma ya haraka kwa wagonjwa wanapo pokelewa kwa vile wengine huhitaji huduma ya dharura .

Hata hivyo wameahidi kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza na kwamba hayatatokea tena.
chanzo: zanzibar24

Comments