Jana nchi ilizizima baada ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi zinazoelezwa kuwa 32 mjini Dodoma.
Mazungumzo
katika mitandao yalichukuliwa na tukio hilo kila mmoja akiomwombea
mbunge huyo baada ya risasi tano kuingia katika maeneo mbalimbali ya
mwili wake.
Watu maarufu hawakubaki nyuma kuelezea
hisia zao kwa tukio hilo na hivi ndivyo baadhi yao walivyoandika katika
mtandao wa Instagram wakiambatanisha na picha yake.
Shilole:
Hatma ya maisha mtu yeyote anayo Mungu na si mwanadamu. Mungu mwenye
kutoa uhai na uzima akupe nafuu mkuu. Watanzania tumeguswa na naamini
una maombi ya wengi sana.
Aunty Ezekiel: Dah!Nakosa la kuongea mwenyezi Mungu tenda miujiza yako.
JB: Naamini Mungu atakuponya na utarudi katika afya yako...Tunakuombea..Mungu atafanya.
Diamond: InshaAllah mwenyezi Mungu akusmamie na kukurudishia afya njema
Irene Uwoya: May you get a quick recovery honourable in God's power....My prayers are with you!!Amen
Idris: At This point tupunguze uchama kuhakikisha Tundu Lissu anakuwa stable, baada ya hapo tutajua nchi imekuwa ya namna gani.
Benpol: Pray for Tundu Lissu
Roma: God. Amen
Jux: #Prayfortundulissu
Lulu: Tuweke
pembeni tofauti ya vyama na maono ya kisiasa...kwa sasa kwa imani/dini
zetu tumuombee kama mtoto wa mama na baba fulani, mume wa mama fulani,
baba mwenye watoto, familia na watu mbalimbali wanaotemgemea.
Tusimuombee Tundu Lissu mbunge au mwanasiasa, tumuombee Tundu Lissu wa
kawaida kabisa kama baba yetu, kaka yetu au mtu yeyote wa kawaida
tunayemjua.
Lady Jay Dee: Mwenyezi
Mungu aliyekuumba akakuinue kutoka kwenye kitanda walichokulaza binadamu
tusiowafamu. Huwa tunaamini kwa jina la baba, la mwana na la roho
mtakatifu.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments