
Septemba, 5 mwaka huu pia wabunge hao walionekana wakigoma na kutoka
nje ya bunge wakieleza kutounga mkono kitendo cha kuapishwa kwa wabunge
Saba wa CUF ya lipumba pia wamefanya hivyohivyo na leo ambapo alikuwa
akiapishwa mbunge mmoja aliyebakia kati ya wale saba walioapishwa.
Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Suzan Lyimo amesema wameamua kutoka nje baada ya kuona ‘Order Paper’ ikionesha kuna Mbunge wa CUF anaapishwa na kusema wataendelea kususia tukio lolote linalohusisha wabunge hao wapya wa CUF.
Kumekuwepo na mgogoro ndani ya CUF hali iliyopelekea kuwepo kwa
makundi mawili moja likiwa ni kundi linalomuunga mkono Mwenyekiti wa CUF
anayetambuliwa na Msajili wa vyama vya siasa Profesa Lipumba, huku
kundi lingine likiwa ni upande wa Katibu Mkuu wa CUF taifa Maalim Seif.
chanzo: zanzibar24.
Comments