Askari
wa jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) aliyefahamika kwa jina la
Praivate Mussa Jumanne Muryery ameuawa kwa kupigwa risasi na kundi la
waasi akiwa kwenye ulinzi wa Amani nchini DRC Congo.
Kwa
mujibu wa taarifa ya (JWTZ) inasema kuwa askari wake huyo alifariki
Septemba 17, 2017 na kufuatia shambulio hilo Umoja wa Mataifa umeunda
bodi ya uchunguzi kuchunguza tukio hilo.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments