
Tukio hilo limetokea Septemba 20, 2017 kwenye bomoabomoa ambayo
inatekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, yenye lengo la kuandaa
eneo ili kupisha mradi mkubwa wa majitaka katika manispaa hiyo.
Wakazi wa eneo hilo wamelalamikia zoezi hilo na kuiomba Serikali
kuwaonea huruma kwani hawana mahali pengine kwa kwenda kujisitiri.
Pamoja na hayo pia eneo hilo la Jangwani lilishapigwa marufuku kwa
wananchi kujengwa makaazi, kwani ni eneo hatarishi kutokana na kuwa
kwenye mkondo wa mto Msimbazi ambao nyakati za masika hufurika.
chanzo: zanzibar24.
Comments