Uchaguzi
mpya wa urais nchini Kenya huenda ukaahirishwa kutoka tarehe 17 mwezi
ujao. Tume ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, imekuwa ikikutana kuangalia
uwezekano wa kuahirisha Uchaguzi huu baada ya kampuni ya Ufaransa ya
Safran Morpho kuomba muda zaidi kuboresha mitambo inayotumiwa kuwatambua
wapiga kura.
Mbali
na hilo, Muungano wa Upinzani Nasa, unaoongozwa na Raila Odinga,
umesema Uchaguzi hautafanyika iwapo marekebisho hayatafanyika ndani ya
Tume ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa Ezra Chiloba
Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo.
Chama
cha Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta kinashutumu shinikizo hilo la
upinzani na kusisitiza uchaguzi ufanyike kama ulivyopangwa.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments