Teu alihudumu kwa nafasi hiyo katika Wizara ya Fedha na baadaye Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, akiwa mbunge wa Mpwapwa.
Akizungumza
leo Jumanne jijini hapa nyumbani kwake Mtaa wa Kaunda eneo la Oysterbay
amesema binti yake Dk Aneth alifanyiwa hafla ya kuagwa mwishoni mwa
wiki iliyopita kabla ya kwenda Uganda kufunga ndoa Jumamosi iliyopita.
Teu
amesema baada ya hafla kumalizika, baadhi ya wanafamilia walipanda
basi na walitangulia kuondoka saa 10:00 jioni kurudi Tanzania.
Amesema yeye, mkewe na baadhi ya watoto walisubiri kupanda ndege saa sita usiku na walifika Dar es Salaam saa nane usiku.
"Tulipokewa
na familia iliyobaki nyumbani, lakini badala ya furaha ilikuwa majonzi
kwa kuwa wenzetu walishapata taarifa kuwa waliotangulia kwa basi
wamepata ajali. Taarifa ilinishtua lakini swali likabaki ni nani na nani
waliofariki kwenye ajali hiyo," amesema.
Teu amesema
baada ya muda walipata taarifa kamili za waliofariki baadhi wakiwa ni
baba yake mzazi na kijana wake wa kwanza, Sakazi Teu.
Amesema
miili ya ndugu zake itawasili Dar es Salaam leo usiku na kuhifadhiwa
katika Hospitali ya Jeshi Lugalo ambako itaagwa kesho asubuhi
hospitalini hapo na baadaye itasafirishwa kwa maziko yatakayofanyika
Mpwapwa na Kilimanjaro.
"Kama familia tumekubaliana
mazishi kufanyika wilayani Mpwapwa ambako ndiko kwetu siku ya Alhamisi
ambako itazikwa miili sita. Ijumaa itakuwa mazishi ya Kilimanjaro ambako
ni miili saba," amesema Teu.
Amesema binti yake
waliyekwenda kumuozesha Dk Aneth Teu na mumewe Dk Trease Ibingira na
ndugu wanane kutoka familia ya Profesa Ibingira ambaye ni mkwewe
watawasili nchini leo.
Amesema binti yake amemaliza
masomo ya udaktari wa binadamu katika Chuo cha KCMC walikokutana na
mumewe ambaye pia alikuwa akisoma udaktari.
Teu ameishukuru Serikali ya Uganda kwa ushirikiano waliotoa ikiwemo kukodi ndege ya kurudisha miili hiyo nchini.
Pia,
ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ikiwemo kukodi magari
mawili kwa ajili ya kusafirisha miili hiyo na eneo la kuihifadhi katika
Hospitali ya Jeshi Lugalo.
chanzo:Mwananchi.
chanzo:Mwananchi.
Comments