Tetemeko kubwa la ardhi laikumba Mexico.

Tetemeko kubwa la ardhi la nguvu ya 8 katika vipimo vya richa limetokezea katika pwani kusini mwa Mexico.

Kitovu cha tetemeko hilo lilitokea umbalia wa karibu milimita 100 kusini magharibi mwa mji wa Pijijiapan katika kina cha kilomita 35, kwa mujibu wa idara ya hali ya hewa ya Marekani.

Onyo la kutokea tsumani limetolewa nchini Mexico, Guatemala, El Salvador, Costa Rica, Nicaragua, Panama na Honduras.


Tetemeko hilo lilisikika katika mji wa Mexico City ambapo watu walitoka majumbani mwao kwenda barabarani.

Mgeni mmoja katika mji huo Luis Carlos Briceno, aliliambia shirika la Reuters, “sijawai kuwa popote pale ambapo ardhi ilisonga sana.”

Umeme umeripotiwa kupotea sehemu za mji.

Hakuna onyo la tsunami lililotolewa pwani magharibi mwa Marekani.

Mexico kwa sasa inatishana na kimbuga mashariki mwa pwani yake.

Kimbunga hicho cha kiwango cha kwanza kipo umbalia wa killomita 300 kusini mashariki mwa Tampico na kimepata kasi ya kilomita 140 kwa saa.

chanzo: BBC na  zanzibar24.

Comments