
Akifungua mkutano wa mwisho wa Jumuiya ya nchi za ACP inayofadhiliwa
na Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi.
Asha Abdalla Ali alisema imefanikiwa kupanga mikakati kuhakikisha dawa
zote zinazoingia nchini ni salama kwa matumizi ya binadamu.
Alisema Jumuiya imewajengea uwezo wafamasia kwa mafunzo mbali mbali
ya kuboresha upatikanaji, usambazaji na kusajili dawa zinazoingia ili
kuhakikisha zilizokuwa chini ya kiwango haziingizwi nchini.
Katibu Mkuu aliongeza kusema kuwa Jumuiya ya nchi za Ukanda wa
Afrika, Carbean na Pacific imefanya juhudi ya kuimarisha Bodi ya
Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar na kuhakikisha inatekelezaji majukumu
yake kwa ufanisi.
Aidha aligusia kuwa Jumuiya imeiwezesha Serikali kufanya mapitio ya
sera yake ya dawa ili kuona inaendana na wakati wa sasa kwa mujibu wa
mahitaji na kuimarisha afya za wananchi.
Bi. Asha alilishukuru Shirika la Afya Duniani na Jumuiya ya nchi za
ukanda wa Afrika, Caribean na Pacific kwa misaada yao mikuwa katika
kuimarisha mifumo ya ufamasia nchini.
Akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo kwa niaba ya mwakilishi wa
Shirikala Afya Duniani nchini Tanzania, mwakilishi wa Shirika hilo
Zanzibar Dkt. Ghirmay Andemichael alisema jukumu la kuwa na dawa salama
katika nchi linahitaji mashirikiano ya wadau mbali mbali ikiwemo
taasisi za serikali, viwanda vya uzalishaji na waingizaji dawa.
Akizungumza katika mkutano huo, Mfamasia Mkuu wa Serikali ya Muungano
wa Tanzania Hendry Kigunde alisema Jumuiya imetoa msukumo mkubwa katika
kipindi cha miaka mitano tokea ilipoanzishwa kwa kuimarisha usambazaji
wa dawa kwa njia za kisasa.
Alisema Serikali imefanikiwa kuboresha miongozo ya uingizwaji wa dawa
na kuoredhesha dawa muhimu ambazo waingizaji wanashauriwa kuzipa
kipaumbele kwa ajili ya matimizi ya wananchi.
Mkutano huo wa siku mbili utafanya mapitio katika kipindi cha miaka
mitano cha Jumuiya ili kujua mafanikio yaliyopatika katika kutandika
mifumo sahihi ya dawa kwa nchi wanachama na kufahamu changamoto
zilizojitokeza katika kipindi hicho.
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
chanzo:zanzibar24.
Comments