Katika
sura ya kwanza kwenye mchakato huo Bulembo ambaye ni mbunge wa
kuteuliwa, Machi 9, alisema hatagombea tena nafasi hiyo mbele ya kikao
cha Baraza la jumuiya hiyo mjini Dodoma. Pia, alitumia fursa hiyo
kuwaaga wajumbe akisema hoja si ubunge alioteuliwa, bali ni utamaduni
aliojiwekea katika maisha yake.
Sura ya pili
ilijionyesha Julai 2, baada ya mwenyekiti huyo kuchukua fomu katika
mazingira yaliyodaiwa kuwa na usiri, akieleza kutii shinikizo lililokuwa
likitolewa na wazee, viongozi na wanachama wa jumuiya hiyo kumuomba
agombea kutetea nafasi yake.
Hata hivyo, akizungumza na
waandishi wa habari juzi katika makao makuu ya ofisi hizo, Bulembo
aliibuka na sura nyingine akielezea kurejea msimamo wake wa kutogombea
na tayari ameshaandika barua aliyoiwasilisha kwa Katibu Mkuu wa chama
hicho, Abdulrahman Kinana.
“Leo (juzi) nitawasilisha
barua yangu kwa katibu mkuu, sitagombea tena ila kwa kuwa bado ni
mwenyekiti hadi siku ya uchaguzi nitabakia kwenye kazi ya kusimamia na
kuchuja wagombea.
Awali, nilichukua fomu baada ya kushinikizwa na makatibu wakuu na wazee bwana chukua fomu nikasema tatizo ni fomu tu basi nikachukua,” alisema Bulembo.
Awali, nilichukua fomu baada ya kushinikizwa na makatibu wakuu na wazee bwana chukua fomu nikasema tatizo ni fomu tu basi nikachukua,” alisema Bulembo.
Alisema licha ya
kuchukua fomu hiyo, bado hakuwapigia simu makatibu hao kuomba msaada kwa
kuwa msimamo wake ni kuwapisha wengine waongoze.
Bulembo
alisema jumuiya hiyo anaiacha katika hali nzuri akiwa amepunguza deni
la Sh4.8 bilioni kwa asilimia 65, kununua pikipiki nchi nzima, kuanzisha
mradi wa jengo la ghorofa 14 jijini Dar es Salaam na kumaliza kesi 130.
Kuhusu uchaguzi, Bulembo alisema matawi manne kati ya 23,435 bado
hayajamalizia uchaguzi, kata 71 kati ya 4,029 hazijamalizia lakini kwa
upande wa Zanzibar uchaguzi umekamilika katika majimbo yote 54.
chanzo:mwananchi.
chanzo:mwananchi.
Comments