SMZ yatolea ufanunuzi tatizo la ukosefu wa Mafuta.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema tatizo la kutoweka kwa mafuta katika sheli za Zanzibar inatokana na kuchelewa kwa meli ya Mafuta iliyotarajiwa kufika September mosi mwaka huu.

Akitowa taarifa kwa  Waandishi wa Habari  Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dk.Juma Muhammed Salum amesema serikali ilichukuwa hatua mbali mbali ikiwemo kusambaza mafuta ya hakiba hadi meli hiyo ilipowasili September 14 ili kupunguza tatizo hilo kwa wamiliki wa Vyombo vya moto.


Hata hivyo amesema serikali kupitia mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nishati ZURA imebadilisha mfumo wa uletaji Mafuta hapa Zanzibar kuazia septemba mosi mwaka huu kutoka katika makampuni manne ambapo kwa sasa itakuwa ni kampuni moja itakayoshinda zabuni.

Amesema kwa  chini ya utaratibu huo utawezesha mafuta kuletwa moja kwa moja Zanzibar baada ya utaratibu wa awali wa mafuta kuchukuliwa kutoka dare s salaam na Mombasa.

Aidha amesema mpaka sasa  kampuni inayohusika kuleta mafuta ni kampuni ya AUGUSTA ENERGY kutoka Switzerland.

Kutokana na utaratibu huo mpya serikali imesema itakuwa na utaratibu wa kutangaza zabuni kila baada ya miezi miwili na kuruhusu kampuni itayoshinda zabuni hiyo  kuendeleza uletaji mafuta hapa Zanzibar.

Hivi karibu wamiliki wa Vyombo vya moto walikabiliwa na Tatizo la ukosefu wa Mafuta katika vituo vya kununulia Mafuta na kupelekea msongamano mkubwa wa Vyombo vya Moto katika vituo vya mchanzo:Zanzibar24.

Comments