SMZ yaombwa kupunguza tozo ya lesseni kwa wafanyabiashara wadogo.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  imetakiwa  kupunguza  tozo ya lesseni ya  biashara  kwa wafanyabiashara wadogo  ili kuwapunguzia gharama kutokana na mitaji yao  hailingani  na  kiwango wanachotozwa na halmashauri.

Akijibu swali katika kikao cha baraza la wawakilishi Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa  na Idara Maalum za SMZ Shamata Shaame Khamis amesema Serikali imezingatia  kiwango cha mtaji  wa mfanyabiashara  na  ada   ambavyo anatozwa kuwa ipo sawa na haimuathiri mfanyabiashara wowote.

Hata hivyo amesema  hakuna tozo kubwa wanaotozwa  kwani  mfanyabiashara  wa kawaida anatozwa kiwango cha Elfu 25 kwa mwezi kwa ajili ya lessen  ya biashara na kwa wafanyabiashara  wadogo kama mamantilie hutozwa  ada ya kuchangia  gharama za usafi na si malipo ya lesseni.
Amesema licha ya kuwa serikali imeweka kiwango hicho cha ada kwa wafanyabiashara lakini bado ni kidogo ukilinganisha na gharama zinazotumika katika shughuli mbalimbali  hivyo ipo haja ya kuongezwa kwa ada  ili kuziongezea  halmashauri  uwezo na kupunguza  utegemezi  wa fedha kutoka serikali kuu.
chanzo:zanzibar24.

Comments