SMZ yaahidi kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wanaokiuka taratibu.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itawachukulia hatua za kisheria viongozi wanaojimilikisha ardhi kinyume na utaratibu ili kupunguza kesi za ardhi zinazoengezeka katika jamii.

Akijibu swali la Nyongeza katika Kikao cha Baraza la wawakilishi Chukwani Nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar,Naibu Waziri wa Ardhi Maji,Nishati na Mazingira Juma Makungu Juma amesema Mapaka sasa wananchi wamekuwa na mwamko mkubwa wa kutumia Ardhi kwa kufuta sheria lakini baadhi ya viongozi wamekuwa wakikiuka utaratibu huo.

Amesema kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya Baadhi ya Viongozi kutumia vibaya kazi zao serikali itaendelea na jitihada za kuwatafuta viongozi hao ili waweze kuchukuliwa hatua jambo ambalo litachangia kuondoa Migogoro ya ardhi katika jamii.
Aidha amesema kutokana na Migogoro ya ardhi kuendelea kuwepo katika jamii kamisheni ya ardhi itaendelea na utaratibu wa kutoa Elimu ya matumizi bora katika jamii kuanzia kwa wananchi ,Masheha ,Wakuu wa mikoa na wa Wilaya ili wananchi waweze kunufaika na rasilimali za Nchi yao.
chanzo: Zanzibar24.

Comments